“hamsini , hamansini , mia.”
“kumamae zenu nyie watoto, nendeni mkahesabu matako ya mama zenu.”
Alifoka mrembo huyo .
Lakini watoto hao ndio kwanza walicheka , wakaendelea kuhesabu huku wakimfuata nyuma nyuma.
“hamsini , hamnsini mia.”
Waliendelea kuhesabu , akisimama nao pia wana simama , alijaribu kuokota jiwe na kuwatisha kuwabonda lakini wapi , walirudi nyuma kidogo alafu wakamfuata tena .
“hamsini hamsini mia .”
Mrembo huyo litamani kulia , akisema ajikaze matako yake yasitikisike anapotembea ilishindikana.
“boda! Boda! , boda!”
Aliita mrembo huyo, piki piki ilikuwa ikikatisha bara barani , alitoka kwenye kichochoro hicho na kuikimbilia, hapo sasa matako yake yalikuwa yakitikisika mara mbili.
“weraaaa weraaaaaaaa.”
Watoto hao walishangilia , jinsi ambavyo tako hilo lilikuwa likitikisika ilikuwa balaa tupu.
“nikupeleke wapi?”
“nyumbani, ila hela atakupa ,Ali.”
“Ahh kumbe we demu wa , Ali , huna haja ya kulipa hii piki piki ni yake.”
Aliongea dereva huyo wa boda boda .
“eh asante Mungu , tulikuwa tumetulia ghettoni kwake polisi wakaja wakaanza kumkimbiza .”
“hiyo kawaida polisi huwa wanamkimbiza kila siku, lakini hawawezi kukamata na hata wakimkamata hamalizi hata siku anatoka .”
Aliongea dereva boda boda huyo , kisha mrembo huyo alipanda kwenye piki piki.
“jinsi tako lake lilivyokuwa limejimwaga kwenye boda boda hiyo alipokaa, basi ndio ilikuwa balaa, watoto wale ndio walishangilia zaidi hata ya mwanzo na kuwakomeshea Yule boda boda alipiga nyimbo yenye sebene la taarabu , basi mrembo huyo nae akalitikisa tako hulo makusudi
“weeeee , kantangazeeeee!!!!”
Watoto hao walipiga yowe na kushangilia huku mrembo huyo akizidi kulitikisa tako lake boda boda hiyo ilipokuwa ikitokomea bara barani.
***
Ali alikatoka mkuku alikatiza kichochoro hiki na kuingia kile polisi walikuwa nyuma nyuma, wakimkimbiza japo hawakuweza kwenda kasi kama alivyokuwa akienda yeye , na wala haikuawachukua muda mrefu tayari walishapotezwa na vichochoro.
“habari , yako sisi ni maafisa wa polisi , umemuona mwanaume mmoja akikimbia hapa?”
“nani Alli?”
“ndio alli , ameelekea wapi?”
“sijui.”
“umejuaje kwamba tunamuulizia yeye?”
“ ni yeye peke yake ndio anakimbizwa na polisi kila siku katika maeneo haya kila siku.”
Aliongea mwanamke huyo aliyekuwa amekaa barazani kwenye mkeka.
Polisi hao waliondoka hapo huku wakilaani na kuenedelea kuulizia watu mbele , lakini hakuna aliyewapa ushirikiano.
Mwisho wakachoka na kuharisha zoezi la kumkimbiza wakarudi mpaka walipopaki gari yao na kurudi kituoni.
“ndio, hapo bibi we , mwanaume asiye na pesa wa kazi gani ?”
Ilisikika sauti ya mrembo aliongea kwenye korido ya nyumba kubwa iliyokuwa na vyumba chungu mzima ,
“halo ya pesa , mwanaume suruali ina husu?”
Mwanamke mwingine aliitikia kwa kuongea kishambenga na kisha zilisikika sauti zingine za wanawake kibao , wakishangilia na kutoa misemo mbali mbali ya mtaani iliyokuwa ikiunga mkono maada hiyo.
karibu kila chumba katika nyumba hiyo alikuwa anaishi mtu tofauti na walikuwa ni watu walio katika mchanganyiko wa rika.
Kuna vijana mabachela , vijana waliooa , wazee mabachela na wazee walioa. Wote waliishi katika nyumba hiyo huku kila mmoja akiwa na itikadi zake , chumba hiki utasikia muziki wa injili ukipiga nyimbo za kumsifu bwana yesu kristo.
Kinachofuata utasikia mnanda na mchiriku , kingine bongo fleva , kingine hip hop.
No comments:
Post a Comment