BY D.G.LWASYE ‘GIFT KIPAPA’
WHATSAP: +255 715 557 191
EMAIL: giftkipapa@gmail.com
Tafadhari heshimu kazi ngumu
ninayofanya, huruhusiwi kunakili na kupost simulizi yangu katika website, page
wala whatsap group lako, stori zangu zote zimesajiliwa matumizi yoyote ya
simulizi hii bila idhini ya Gift kipapa ni kosa kisheria.
MWANZO WA STORI:
Mtaa ulikuwa kimya ndege tu ndio waliosikika wakiiimba kila
upepo ulipovuma , gari moja la kifahari lilikatisha katika mtaa huo na
kuyafanya majani ya miti yaliyokuwa yamedondokea barabarani yapeperuke kimo
Fulani gari hilo lilipopita majani hayo yalidondoka chini tena.
Na harafu ukimya
ulitanda tena . kando kando ya bara bara hiyo kulikuwa na nyumba za kifahari
zilizozungushiwa kuta nene, pamoja na bustani za maua mazuri ya kupendeza.
Dakika kumi na tano baadae bajaji iliiibuka katika mtaa huo
ilkwenda mwendo waka kasi , japo haikuwa kasi kama ile ambayo lilipita lile
gari, nyumba ya kwanza ya pili ya tatu , bajaji hiyo ilipunguza mwendo , na
kisha huyu mvulana aliyekuwa amevalia ovaloli lililoandikwa clean! Clean! Alishuka , bajaji hiyo iliondoka na yeye
alipiga hatua kusogelea geti kubwa lililokuwa
mbele yake.
Alibonyeza kengele na kusubiri kwa sekunde kadhaa kisha
sauti kutoka kwenye kipaza sauti cha kengele hiyo ilisikika.
“jina lako nani?na ni nini kimekuleta hapa?”
Ilisikika sauti ya mwanamke .
“shadrack , natoka katika kampuni ya usafi , clean clean.”
Aliongea mwanume huyo.
“oh shadrak ! ingia nilikuwa ninakutarajia.”
Aliongea m,wanamke huyo na kihs geti lilifunguka lenyewe ,
shadrack aliiingia na kisha geti hilo lilijifunga.
Nyumba hiyo kubwa iliyokuwa na bustani nzuri ilimfanya
shadrack astaajabu kwa dakika kadhaa.
Alipiga hatua kuelekea ulipomlango wa kuingilia ndani , na
kmwkwenye mlangio huo kulikuwa na mwana mama wa makamu , aliyekuwa anamsubiri .
‘nilifikiri watawatuma wawili , utaweza kufanya kazi zote
opeke yako?”
Aliuliza mwanamke huyo huku akimuangalia shadrack usoni.
“ndio maana wamenituma mwenyewe.”
Aliitikia shadrack, huku akimuangalia mwana mama huyo usoni
mara baada yta kufika pale aliposimama , macho yao yaligongana na uso wa mwanamke
huyo ulikuwa na tabasamu lililofifia.
“sawa shadrsk , nataka kuuona uhodari wako , stoo ipo kwule kwenye nyumba ya nje mlango wa tatu
hii ni funguo yake , utaopata vuifaa vyote unavyohitaji.’
Aliongea mwana mama huyo.
“ahsante bibie.”
Shadrack aliitikia huku akipokea funguo hizo.
Alitembea kuelekea kwenye nyumba ya nje iliyokuwa umejitenga
kwa umbali Fulani hivi toka ilipo nyumba
kubwa , nia ya kuelekea huko ilikuwa imesakagfiwa kwa zege huku pembeni kukiwa
na viwanja vyenye nyasi zilizokatwa vizuri
na mwanaume ambae alikuwa akishughulika na mashine ya kukatia nyasi
upande huo wa nyumba ya nje , mashine yake ilikuwa ikipiga kelele lakini
mwanaume huyo alikuwa amezoea .
Upande mwingine kulikuwa na mpira wa maji uliokuwa umefungwa
kifaa cha kumwagilia kilichokuwa kikirusha maji kwenye majani hayo kila upande
zamu kwa zamu.
Shadrack alipofika kwenye nyumba hiyo alisogelea mlango
alioelekezwa na kufungua , alipoingia ndani alijikuta anastaajabu, kila kifaa
kinachotumika kwaajili ya usafi kilikuwa humo , kuna baadhi ya vifaa hata
ofisimni kwao havikuwemo, kwa kweli hakuamini vifaa bora kama hiovyo vinawea
kufungiwa ndani kusubiri kufanya kazi ya nyumba moja kwa muda wote huo , kila
kifaa alichokiona humo kilikuwa ni ndoto ya mfanya usafi yoyote ulimwenguni
hata bosi wake alikuwa akiviota vifaa hivyo.
“unahitaji msaada?”
Ilisikika sauti hiyo iliyomshtua shadrak. Aligeuka haraka
kumuangalia mtu aliyeongea .
Alikuwa ni yule mwanaume aliyemuona kwambali akikata nyasi
na mashine.
“oh , Mungu wangu umenishtua.”
Aliongea shadrack na kumuangalia mwanume huyo usoni.
Mwanaume huyo alimuangalia nae pia.
‘mambo , naitwa shadrack.”
Aliongea shadrack.
“safi shadrack , vipi unahitaji msaada?”
No comments:
Post a Comment