NOT YOU NOW! SE 1 EP 02


Hakuna aliyejua sababu ya kengele hiyo kulia si kilanja mkuu wala mgonga kengele mwenyewe yeye alifuata amri tu aliyopewa na mkuu wa shule.
Ni Joel pekee ndio alikuwa ana hisi hisi tu kwamba huenda ujumbe wake umemfikia mkuu wa shule.
Wanafunzi wote walijipanga kila kidato na mstali wake , walikaa kimya ilikujua kinachoendelea.
Jukwaani alisimama mkuu wa shule na mwalimu wa taaluma, muonekano wa mkuu wa shule uliwatisha wanafunzi wote, uso wake ulikuwa umekunjamana kwa hasira. Jambo hili lilimfanya joel apate uhakika kwamba sasa ujumbe wake umefika.
Kilanja mkuu aliitwa na kukabidhiwa karatasi  awasomee wenzake kilichoandikwa katika karatasi hiyo, alianza kusoma.
“kwako mkuu wa shule , shikamoo, mimi ni mwanafunzi wako naleta malalamiko yangu juu ya jambo alilotendewa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika mashindano ya kumtafuta mwanafunzi anayeweza kujieleza vizuri katika mdahalo kwa lugha ya kiingereza.
Grace Samson mwanafunzi wa kidato cha kwanza amejieleza vizuri sana na ametoa hoja ambazo kama angepewa nafasi ya kuiwakilisha shule yetu katika mashindano hayo nje ya shule nina hakika angeweza kuleta sifa ambayo kwa hakika shule yetu ingejivunia kuwa naye, lakini kwa kuwa majaji wa shindano hilo walikuwa ni wanafunzi wa kidato cha nne basi wameamua kufanya maamuzi wanavyojua kwa kumpatia mwanafunzi mwenzao wa kidato cha nne aitwaye fatuma Abdalla nafasi hiyo wakati hana uwezo mkubwa kama ilivyo kwa Grace Samson.
 Nimesikitishwa sana na maamuzi haya mkuu, na nina hoji kwamba kuna haja gani ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kuwekwa kwenye mashindano hayo kama watasimama kama vivuli tu? 
Si kawaida kwa shule zetu hizi za serikali ambazo wanafunzi wake wengi wanatokea shule zetu za msingi ambazo zinatumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia kuweza kuzungumza na kujieleza vizuri lugha ya kiingereza  kama ambavyo Grace Samson ameweza , bali wengi wanakuwa wakitatizwa na lugha hiyo mpaka kufikia kidato cha pili hadi cha tatu hivi, lakini leo hii mwanafunzi wa kidato cha kwanza ameonyesha uwezo huo na alichoambulia ni kuvunjwa moyo na kupokonywa haki yake.
Ni hayo tu mkuu nimeandika kwako kwa kuwa najua wewe ndio mkuu wa shule hii na ndio mwamuzi wa mwisho katika masuala yote yanayoendelea katika shule hii ili uweze kuliangalia jambo hili na kuhakikisha haki inatendeka, Ahsante.”
Alimaliza kusoma kilanja mkuu.
Wanafunzi wote walishikwa na bumbuwazi huku wote wakiwa wamegeuza vichwa vyao kumuangalia Grace kwani kila mmoja aliamini Grace ndio aliyeandika barua hiyo.
“Ni nani aliyeandika barua hiyo?”
Aliuliza mkuu wa shule , wanafunzi wote walibaki kimya
“narudia tena swali langu , ni nani ameandika barua hiyo?”
Aliuliza tena mkuu wa shule macho ya wanafunzi wote yalikuwa kwa Grace.
“mimi ndio nimeandika.”
Sauti hiyo iliposikika wanafunzi wote waligeuza vichwa vyao kumuangalia mtu aliyeitoa kauli hiyo,  hakuna aliyeamini baada ya kumuona Joel akijitokeza.
“Ni Joel!, jamani mungu wangu!”
ilisikika sauti ya msichana mmoja aliyeongea kwa masikitiko, kwani walichoamini wanafunzi wote ni kwamba Joel amefanya kosa kubwa. Ambalo linaweza kumfanya afukuzwe shule au kupewa adhabu kali. Walifikiria hivyo kwa sababu walimfahamu vyema mkuu wao wa shule, alikuwa hapendi mzaha hata kidogo, alikuwa haoni hasara kumfukuza shule mwanafunzi hata kama akifanya kosa hata kidogo, kesi ikimfikia yeye tu basi hakukuwa na msamaha.
Wapo wanafunzi waliofukuzwa kwa kutovaa tai, soksi na hata kutochomekea shati sembuse yeye ambaye alifikia hatua ya kumuandikia barua kabisa.
Joel aliyajua yote hayo lakini tayari alikuwa ameshaamua kujitoa mhanga, alikuwa tayari hata kufukuzwa shule lakini sio kuiona haki ya Grace inapotea.
Alijitokeza mbele ya jukwaa, wanafunzi wote walikuwa wakimuangalia kwa huruma. Upande wa Grace ndio machozi yalikuwa yakimbubujikka mashavuni , aliumia kuona mtu anataka kufukuzwa shule kwa sababu yake.
Mkuu wa shule alimuangalia Joel na kisha kutoa tabasamu usoni mwake na tabasamu hilo lilikuwa la kwanza tangua aliposimama katika jukwaa hilo ahsubuhi hiyo.
“mpigieni makofi.’
Mkuu wa shule aliamrisha, nukta hiyo hiyo wanafunzi wote walipiga makofi huku wakiwa hawaelewi kwa nini mkuu kawambia wafanye hivyo.
“Vizuri.”
Mkuu wa shule aliongea mara baada ya wanafunzi kumaliza kupiga makofi hayo.
Alikaa kimya kwa nukta kadhaa na kisha kuanza kuongea tena.
“huyu ni mfano wa kuigwa , katika shule yangu hajawahi kutokea mwanafunzi mwenye ujasiri na mpenda haki kama ilivyo kwa kijana huyu.”
Aliongea huku akimuangalia Joel usoni alimpa mkono na Joel aliupokea mkono huo na wakasalimiana kwa mara ya kwanza na mkuu wa shule tangu aanze masomo yake miaka mitatu iliyopita.
“hongera sana kijana kwa ujasili wako.”
Aliogea mkuu wa shule huku bado wakiwa wameshikana mkono.
“ahsante mkuu.”
Aliitikia Joel japo wasi wasi bado ulikuwa haujatoka mwilini mwake.
Mkuu wa shule baada ya kumaliza kupeana mkono na Joel, aliwageukia wanafunzi , ambapo aliwaita majaji wa shindano hilo na kuwakaripia sana , alimgeukia mwalimu wa taaluma naye pia alimkaripia kwa kuacha tukio kubwa  kama hilo lifanywe na wanafunzi wenyewe japo yeye alijitetea kwamba alikuwa na dharula iliyompelekea kutofika kabisa shule siku hiyo.
Hakuishia hapo uongozi wote wa wanafunzi ulikaripiwa mno.  Alimuita Grace mbele akampa pole na kisha akataka pambano hlo lirudiwe muda huo huo na yeye akiwepo, vipindi pamoja na shuguli zote za kiofisi zilisimamishwa kwa muda kisha alitaka wanafunzi wote , walimu pamoja na wafanyakazi wa shule wote wepo katika mpambano huo.
Yani ilikuwa kama baraza la shule ambalo huwa linafanyika mara moja tu  kwa muhula.

UNATARAJIA NINI KATIKA MPAMBANO HUU WA KIHISTORIA KUWAHI KUTOKEA KATIKA SEKONDARI TUKUYU?

No comments:

Post a Comment