(hadithi ya mwanamke aliyepoteza mwelekeo lakini mapenzi yalimuongoza mpaka nyumbani)
Kabla ya vita alikuwa akitumia utashi wake kusimamia mambo ambayo sasa anayona ni ya kipuuzi, anahisi wakati huo alikuwa hafahamu lolote na wala ulimwengu haukuwa na maana yoyote kwake.
Lakini sasa anaamua kutumia utashi wake kwa jambo moja tu , jambo ambalo ni kutimiza ahadi aliyompa mwanume anayempenda kuliko kitu chochote katika maisha yake , kwamba kama ulimwengu hautaisha katika kipindi cha vita anataka kuwa nyumbani na yeye kwasababu hivyo ndivyo anavyoishi sasa.
Bila shaka unataka kumfahamu msichana huyu.
Jina lake ni Elithabeth lakini hakuna anayemuita jina hilo kasoro baba yake tu ambaye yeye anamuona ni mpuuzi. yeye mwenyewe anapenda kuitwa Daisy,msichana huyu wa kimarekani alizaliwa siku ambayo mama yake alifariki, jambo hilo limekuwa likimfanya ajihisi mwenye hatia wakati Fulani katika maisha yake kwa kuhisi kwamba kama yeye asingelizaiwa basi mama yake angekuwa hai hadi leo.
Na zaidi ya hayo amekulia katika mazingira ya kutoelewana na baba yake kwa kipindi kirefu . kwa sababu anaamini baba yake hampendi , na wala hamjali.
Katika likizo ya msimu wa kiangazi aliamua kusafiri mpaka uingereza kwa shangazi yake ili atumie muda huo na binamu zake. Msimu huo wa kiangazi haukuwa wa kawaida kwa Daisy bali msimu ambao unakwenda kubadilisha kila kitu katika maisha yake, ikiwa ni pamoja na kulipata penzi la kweli kwa mara ya kwanza katika maisha yake , kufahamu ukweli zaidi kuhusu mama yake mzazi na hata kujua jinsi ambavyo ilivyo kwa mtu kukimbilia sehemu usiyoijua , pasipo kukoma ili tu upate nafasi ya kuendelea kuishi.
Aliposimama kwa mara ya kwanza katika kiwanja cha ndege nchini uingereza Daisy alimuona mvulana mdogo aliyevalia miwani ya macho akiwa ameshikilia bango lililoandikwa jina lake, alipomsogelea mvulana huyo ali msabahi
“habari”
“wewe ni yupi kati yao?”
Aliuliza
“mimi ni Isack!” mvulana huyo alijibu kwa bashasha pasipo kujua jinsi jina Elithabeth liloandikwa kwenye bango alilolishikiria linavyomkera Daisy.
“hakuna anayeniita Elithabeth kasoro baba yangu ambaye naye ni mpuuzi, kwa hiyo kama hutojali unaweza kuniita daisy”
“Daisy ,safi sana” isack aliitikia
“mama yako yuko wapi?”
“ametingwa na kazi hivyo amenituma mimi nije kukuchukua”
Hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kumuona binamu wake huyo , na kwa mara hiyo tu daisy alianza kuzionyesha tabia zake za kiubaguzi kwani hakutaka hata isack ambebe begi japo lilikuwa zito .
Walipanda gari kuelekea katika makazi yao yaliyopo nje ya mji kwenye kilima kilichozungukwa na msitu .
Japo awali daisy hakuta kupanda gari hilo kwa kuofia kuendeshwa na isack kwa kua bado mdogo lakini badae alikubali baada ya kugundua kwamba hakuna usafiri mwingine ka siku hiyo zaidi ya gari hilo.
Walpofikia karibu na nyumbani kwao daisy akiduwaa kumuangalia mvulana mmoja aliyesimama kando ya barabara akiwa ameshika mwewe. Hakusikia sauti yoyote toka moyoni mwake inayo mweleza jambo kuhusu mvulana huyo , bali macho yake yalikuwa kama vile yamenaswa na sumaku toka kwenye macho ya mvulana huyo, na muonekano wake bila shaka, ungeweza kumfanya msichana yoyote azubae kumuangalia, alikuwa ni mzuri kwa kweli.
Gari liliposimama daisyalishuka na mizigo yake. mbwa wa familia alimrukia kumraki lakini daisy alifoka akita mbwa hao wakae mbali naye kila mtu alijaribu kuwazui mbwa hao lakini hawakuacha, mpaka wakamdondosha chini , na hapo Yule jamaa aliyekuwa ameshika mwewe akaja na kuwatoa mbwa hao. Akanyoosha mkono kumpatia Daisy ili amuinue, siwezi kuelezea jinsi Dasiy alipojisikia mara tu baada ya kuupata mguso wa mwanaume huyo , kitu pekee nachoweza kusema ni jinsi macho yao yalivyo gongana hakuna yoyote kati yao aliye kuwa tayari kupepesa macho yak e kwa wakati huo. Kilichofuata unajua mvulana huyo alipomaliza kumuinua Daisy alianza kupiga hatua na kuondoka .
Daisy alitamani mvulana huyo aendelee kubaki hapo.
“subiri kidogo” daisy alijaribu kumsimamisha lakini huyu jamaa wala hakusimama aliendelea kutembea mpaka alipotokopea msituni.
“ni nani Yule?” alimuuliza isack
“Edmond. Yeye ndiyo mkubwa,”
Isack aliitikia ,
Na kwa Daisy huu haukuwa utambulisho wa binamu wake pekee bali ni utambulisho wa mwanume ambaye atamfanya autazame ulimwengu katika muonekano tofauti, kwa sababu penzi litazuka kati yao na ni kwa wakati huo ndiyo ataionja ladha ya maisha ya furaha , lakini jambo hilo halikudumu kwani hicho kilikuwa kipindi ambacho serikali ya uingereza ilipoingia katika mgogoro na waasi , mgogogoro ulioshindwa kutatulika mezani na kuzua vita vilivyo sababisha na nchi hiyo kuongozwa na jeshi ambapo jeshi liliamua kuwaamisha watu wote katika maeneo ambayo waasi wameyakaribia, uhamishaji huo ulizitenga familia, wanaume kwao na wanawake kwao na yoyote atakaye kaidi atakumbana na mtiti wa jeshi.
Ni wakati huo ndio Edimond alikuwa na ombi kwa Daisy.
“popote watakapokupeleka , niahidi utatafuta njia ya kurejea hapa”
Hilo ndilo lilikuwa ombi la Edmond lililo mfanya Daisy atoe ahadi kwamba
“kama ulimwengu hautaisha nataka kuwa hapa nyumbani na wewe na hivi ndivyo jinsi ninavyo ishi sasa”
Na huo ndio ukawa mwanzo wa mshike mshike ambao kama ukiangalia wewe mwenye utaona jinsi ambacho mwanamke anaweza kuthubutu kufanya moyo wake ukipenda.
Alikimbia akiwa amemshika mkono binamu yake mdogo wa kike. Bila kujali milio ya mitutu na sauti za wanaume wenye uchu wa kubaka zikimtisha asimame.
Na kitendo cha kushuhudia maiti ya isack ikiwa inatupwa katikati ya maiti zilizokuwa zimebwagwa kwenye eneo walilopelekwa wanaume kipindi walipowatenga .
Kitendo hicho kilimfanya aukaze moyo na kudiriki kuwafyatulia risasi mpaka kuwauwa wanaume waliokuwa wanataka kuwaumiza na kuwabaka yeye pamoja na binamu yake.
Na hata hivyo filamu hii haiwausu ndege hawa wawili waliopendana peke yao, bali pia utapata kuuona stori ya mwanamama aliyejitoa mhanga kuitumikia serikali, mpaka kuwa na moyo mgumu wa kuitoa kafara familia yake kwa kuitelekeza katika eneo la vita na kuelekea uswiss wakati alikuwa na uwezo wa kuihamisha mapema kabla ya vita hivyo kuanza.
Maskini watoto wake wakiwa na matumaini na mama yao kwamba anafanya kazi ya kuikomboa dunia.
angalia trailer la muvi hii ikiwa na subtitle za kiswahilikwa kubonye link hiyo hapo chini.