Stori ya msichana fundi magari aliyechanganywa na jasusi anayejaribu kulisafisha jina lake.
Akitokea katika jiji la Kansas kununua skrepa za gari June Havens anajikuta katika misukosuko mara baada ya kukutana na jasusi wa kitengo cha siri ambaye yupo katika oparesheni hatari inayoweza kugharimu maisha yake na ya June pia pamoja na maisha ya mwanafunzi wa sekondari ya Juu Simon Felk ambaye alitengeneza Betri lenye chaji isiyoisha na yenye uwezo mkubwa.
Betri ambalo ndiyo chanzo cha vulumai lote kwani kuna wafanya biashara haramu ya siraha wanalitaka betri hilo kwa gharama yoyote ile na kumuua aliye litengeneza huku serikali ikimuwinda jasusi wao Roy Miller kwa tuhuma ya kutaka kuliuza Betri hilo baada ya kulaghaiwa na jasusi mwenzake Fitz ambaye ndiye hasa anayetaka kumuua simon na kuliuza betri hilo. Huku serikali kule wafanya biashara halamu wote wana muwinda mtu mmoja na wote wako tayari kumuua ili mradi betri hilo liwe katika mikono yao.
Hapo ndipo utakapoona utamu wa filamu hii ambayo haina misukosuko peke yake bali pia penzi zito lililoibuka kati ya jasusi Roy Miller na fundi magari June Heaveans.
(UKIITAKA FILAMU HII IKIWA NA SUBTITLE ZA KISWAHILI WASILIANA NASi.)
Director:
James Mangold
Writer:
Patrick O'Neill
Stars:
Tom Cruise, Cameron Diaz, Peter Sarsgaard
James Mangold
Writer:
Patrick O'Neill
Stars:
Tom Cruise, Cameron Diaz, Peter Sarsgaard
No comments:
Post a Comment