RUDI NYUMA EPISODI YA 07
NENDA KWNYE ORODHA YA VITABU.
Shadrack aliwaangalia huku akitikisa kichwa chake ,
hakupenda lolote kati ya hayo, maisha ya washua yalikuwa yamemuingia
kichwani alikuwa anatamani kama siku
moja angeamka na maisha yake yote yawe huko , alikuwa anapenda vile vicheko
vyao, mandhari tulivu muziki wa taratibu
kutoka katika piano inayobonyezwa na mtaalamu wa muziki pamoja na yale maglasi ya wayne wanayo yashikikilia
wakiwa wamekusanyika pamoja kwenye sherehe zao , waliziita dina parti ,
valentine na majina mengine kibao ya kitasha kibao , shadrack alikuwa akiota
hivyo vitu kila siku lakini kitu pekee alichokuwa anakipata ni hizi nyimbo za
kina dogo mfaume na kazi yake ya dukani pamoja na zingine zingine walizotwanga
wakina omari omari na waimba singeli kibao,
pamoja na hivi vihoja vya watu kuvua nguo hadharani kama wehu, bila kujari
watoto wadogo kuwepo jirani , wenyewe waliita kumwaga razi na kweli radhi
ilikuwa inamwagika sio mchezo.
“eeeeh , shadrack, jamaa yangu leo nimekuotea, uniambii
kitu.”
Shadrack aliisikia sauti hiyo na kugeuka kumwangalia mtu aliyemuita ,
alikuwa ni mmoja kati ya wale wanaume waliozunguka duara mule kirabuni.
Domo lake lilikuwa zito na alikuwa akiyumba yumba hivi
kusogea jirani toka kirabuni kumfuata shadrack.
“potonto! kumamako walai huyu mjinga atanisumbua kinoma , sijui hata kwa nini nimepita huku
kirabuni.”
Alilaani shadrack
huku akimuangalia potonto akija
kwa kuyumba nyumba , aligonga meza kadhaa walizokaa walevi wenzake
wakinywa mtungi, nusu amwage mitungi yao , chupa pamoja na mabakuli ya plastiki yaliyokuwa na
pombe hizo yalitikiska tikisika hivi kwenye meza hiyo.
“oya wewe fala angalia unakokwenda , mwangalie kwanza mwendo
wake ka msenge.”
Aliropoka mmoja kati ya walevi waliokuwa wamekaa kwenye meza
iliyotikiswa baada ya pombe yake kumwagika kidogo kwenye meza hiyo.
“ndio ni msenge fresh namfila na mkeo vile vile, kuma wewe “
Alijibu potonto huku akiendelea kutembea.
Shadrack alimuangalia jinsi alivyokuwa anatembea kilevi levi
, mavazi yake jinsi yalivyochoka na hata
sura yake , alikuwa anaonekana mkubwa kuliko yeye , lakini ukweli ni kwamba
walisoma darasa moja toka shule ya msingi
na walikuwa marafiki wakubwa , walicheza michezo yote ya mtaani pamoja
lakini alifeli shule ya msingi wakati shadrack alipo fauli shule ya kata japo
hata yeye hakufanya vizuri zaidi lakini aliishika kusoma chuo cha kutunza
nyumba. Na sasa yupo huko kusafisha nyumba za washua wakati mwenzake ndio kazi
kushinda na mitungi kwenye virabu akibomu kila mtu aliyemjua mpaka kieleweke.
“oya pontonto
inakuaje mtu wangu wa nguvu , mbona umepotea hivyo kitaa nilifikiri
umesafiri?”
Aliongea shadrack
huku akijifanya kuchangamka kinafiki.
“niende wapi mimi jembe langu wakati dar ndio nyumbani.”
Aliongea potonto huku akiyumba yumba hivi kwa kurudi nyuma
kwenda mbele.
“niambie mkali wangu mishe zina kwendaje?”
Shadrack aliongeza.
“mishe kitu gani mkali wangu , mishe mnazifanya nyie huko na
washua, chakufanya nizungushie raundi hapa mimi nijimiminie mitungi barida.”
Aliongea potonto kwa
sauti ya kilevi levi .
Shadrackl hakutaka kufanya nae maongezi nae sana , aliingiza
mkono wake mfukoni haraka na kutoa noti ya shilingi elfu tano na kisha
kumdakisha.
“barida mkali wangu , ndio maana nakukubali shadrack wewe
ndio jembe la maana.”
Aliongea potonto kwa furaha kinoma , lakini alivyochomoka
hapo yani hata maongezi yenyewe na shadrack aliyakatisha, alirudi kirabuni
akiwa na madaha kinoma , shadrack alimuangalia jinsi alivyokuwa anawasukuma
sukuma walevi wenzie humo ndani aliishia kutikisa kichwa chake kwa huruma kinoma.
“oya shadrack , shadrack na mimi nitoe mai tano ,”
Aliongea mlevi mmoja alikuwa amelala chali kwenye kichochoro
hicho suruali yake yote ikiwa imelowa
kwa mkojo .
“embu toka zako huko
lpyana umejikojolea, pombe zitakuua wewe mjinga .”
Shadrack alifoka.
‘eeh na wewe shadrack nipe jero tu, nataka chupa moja tu ya
mwisho, moja tu.”
Aliongea tena mvulana huyo na alafu safari hii alijamba mavi yake yalikuwa yananuka kinoma.
“toka zako huko mwehu wewe.”
Alifoka shadrack huku
akimpita kwa kumruka pale chini sababu alikuwa amejilaza kwa kuziba kichocoro
chote .
Watu wote walipita hapo ilikuwa lazima wamruke yeye.
MWISHO WA KITABU CHA KWANZA.
KWA VITABU ZAIDI WASILIANA NAMI KWA :
WHATSAP: +255 715 557 191
EMAIL: giftkipapa@gmail.com
Tafadhari heshimu kazi ngumu
ninayofanya, huruhusiwi kunakili na kupost simulizi yangu katika website, page
wala whatsap group lako, stori zangu zote zimesajiliwa matumizi yoyote ya
simulizi hii bila idhini ya Gift kipapa ni kosa kisheria.
NENDA KWNYE ORODHA YA VITABU.
No comments:
Post a Comment